MAKALA : WIZI WA ALMASI WA GRAFF DIAMONDS LONDON AMBAZO MPAKA LEO HAZIKUPATIKANA

ASUBUHI NA MAPEMA KWA MTAALAMU WA KUREMBA NA KUTENGENEZA SURA.
Ni tarehe 6 mwezi August mwaka 2009 jamaa wawili wanaingia saluni kwa mtaalamu wa make up. Ni wachangamfu hawana wasiwasi. Mmoja ni mwenye asili ya afrika na mwingine mzungu. Wanaongea na mtaalamu huyo wa make kuwa wanataka wafanyiwe make up ambayo itabadilisha sura na hata rangi zao kuwa za aina ya kipekee yenye mvuto na pia waonekane kuwa umri umeenda eenda kiasi.. yaani watu wazima flan hivi. Kama vile ambavyo huwa unawaona wadada siku ya harusi wanavyopendeza ngozi inaonekana laini, nyororo na yenye weupe wa kuvutia. Jenga picha hiyo kwa jamaa hawa ambao wameenda kwa huyu mtaalamu wa make –up awatengeneze ili waweze kwenda kushiriki kwenye video ya wimbo flan mkali kama ambavyo walimwambia mtaalam.
Jamaa anawaambia msitie shaka hapa ndo mmefika mimi ni mtalaamu wa haya mambo ulizeni hapa London watu wananitambua. Anawaweka kitako na kutaka wa relax na mara anawaita vijana wake waisadizi na kuwaambia wasilaze damu waanze kupiga kazi. Jamaa hawa wametulia sana wanatengenezwa vizuri sana kwa kubandikwa hata ngozi nyingine kwa kitaalam kabisa kutumia latex prosthetics material ambayo ilikuwa inamfanya mtu abadilike na kuwa vile ambavyo angetaka awe kulingana na maelezo. Wao jamaa walitaka waonekane ni watu wazima wenye pesa jinsi ambavyo wangeenda kushiriki kwenye hiyo video ya wimbo wa pop.
Baada ya masaa kadhaa jamaa walikuwa tayari na mtalaam akawaambia wajitizame kwenye vioo… wakajicheki mshkaji mmoja hakuridhika sana na akidai haioeneshi kama ni yenyewe hasa hasa hivyo akaiondoa ile latex na kutaka apakwe tu powder na mambo mambo flani aonekane mtu mzima kweli kweli. Aisee … walikuwa wmaebadilika sana. Bwana mmoja aliyekuwa aliyekuja kufahamika kwa jina la Kassaye akasema huku akitabasamu mbele ya kioo “aisee hapa hata mama yangu hawezi nitambua” mwenzie akacheka na kujibu “ hilo litakuwa jambo zuri sana au siyo?” wakacheka wakapeana tano, wakalipa pesa ya watu wakashukuru na kuondoka.
NINI ILIKUWA SABABU YA UKARABATI ULE WA SURA?
Duka la Diamond la Graff
Siku hiyo hiyo saa 10:40 jamaa wawili waliokuwa wamevalia kinadhifu sana. Wenye kupendeza walifika katika duka kuuubwa la sonara lililokuwa liikitwa Graff Diamonds Jewellery kwa Taxi. Jamaa wale wawili wakatoa pesa kumlipa dereva kwa noti ya paund 20 na nauli mpaka pale ilikuwa ni paund 9.20 wakamwambia atunze change. Hii ilikuwa ni tip kubwa sana kwa dereva Taxi yule kupata. Lengo lilikuwa ni kumfanya dereva taxi yule awaangalie kwa umakini na asisahau sura zao tena. Si unajua kuna mtu anakuachia pesa mpaka unamizama mara mbili mbili kuwa atakuwa nani huyu kuniachia mkwanja kama huu.
Jamaa wawili wanadhifu wakiingia Duka la Almas la Graff
Kwa madaha pasina haraka wakaelekea ulipo mlango wa duka hilo la sonara. Mmoja wa wale wateja waliokuwa wamevalia kinadhifu alikuwa amevaa gloves lakini mlinzi mlangoni hakumzuia kuingia sababu jamaa alikuwa amepigilia vitu vya ukweli hasa.suit kali na alionekana tu kwa macho kuwa alikuwa ni mtu mwenye pesa zake.mwendo wake wa utulivu na majidai, alivyokuwa anaongea jamaa alikuwa amejaa pesa tu .yaani ni wale watu wanaonekana wana mpunga wa ukweli hasa.ukimwangalia hata ngozi yake inaonekana tu. Unajua ukiwa na pesa za ukweli hata ngozi na rangi yako inakutangaza.pesa haijifichi hata kidogo.na walipoingia ndani waliwatishia wafanyakazi kwa silaha walale chini. Na hawakuwa wakihangaika na kuficha sura zisizonekane kwenye cctv camera kwa jinsi ambavyo walikuwa wameweza kujibadilisha sura zile.
Petra Ehnar huyu alikuwa ni mmoja kati ya wauzaji katika duka lile. Walimchukua huyu dada huku wamemshikia bastola na kumwambia awasaidie katika kufungua makabati yenye almasi. Huko wakakusanya jumla ya pete za almas zipatazo 43, Mikufu, bangili na saa. Kwa huo muda wote mhudumu yule alikuwa ameshikwa mateka na wale wezi walimwambia ikiwa asingeonesha ushirikiano au angefanya ukaidi basi wasingechelewa kumwaisha eidha kuzimu au mbinguni kutegemeana na maisha aliyokuwa ameishi hapa duniani. Yaani wange muua. Basi walipomaliza kuyakusanya yale makitu ya thamani wakamtoa yule dada nje ili akapate hewa safi maana ni dhahiri shaili walishamwona yule dada hali yake ilikuwa tete. Baada ya hapo ili kusababisha woga na hofu jamaa walipiga risasi moja hewani. Jamaa waliokuwa ndani wakajificha chini ya soli za viatu vyao kwa woga. Waliokuwa na haja ndogo karibu ilitoka na wengine kuanza kutubu muda huo huo wakijua sasa ndo mwisho wao wa dunia umekaribia.
Baada ya hapo jamaa wale wakatoka na kuingia kwenye kitu BMW ya Blue iliyokuwa imepaki pembezoni mwa mtaa wa Dover. Wakatimka. Wakiwa wanaondoka Kassaye akajitokeza nje ya dirisha na kupiga risasi tatu akielekeza alipo Robert French ambaye alikuwa nje ya pub moja hapo karibu aliye waona hao wezi akadhani walikuwa ni jamaa ambao wamegonga mtu na sasa wanataka kukimbia. Of course alishoot kumtishia tu hakutaka kumuua… maana huyu mshkaji Robert Frenach alijifanya ghafla amekuwa usain bolt na kuanza kuwakimbiza wale wezi kwa miguu.Jamaa wakafanikiwa kutoka eneo lile ila bahati mbaya wakapata ajali waligongana na CAB moja njiani.
BMW rangi ya Blue iliyokuwa amesimamishwa pembezoni mwa Barabara.
So ikabidi Walipofika sehemu nyingine tena washuke na kuicha ile gari wakaingia kwenye Mercedes Benz rangi ya Silverwakachanja mbuga mpaka walipofika mtaa wa Farm huko haikuweza tena kueleweka nini kiliendelea maana watu hawakuweza kujua nini kilitokea walishapotezwa maboya. Wakati huo wa harakati za kutoroka na kukimbia jamaa mmoja aliyekuw akiitwa East Finchley yeye alikuwa amekodi Gari kubwa la tani 7.5 akiwa block Traffic waliokuwa wakiwakimbiza wale washkaji wawili. Ndo hapo unakuta akile kibao MEN AT WORK. ha ha ha. Jamaa wakatokomea huko kwa wanatokomea.
NINI KILITOKEA MPAKA KUFIKIA HAPA?
Tarehe 4 August Kassaye na Calderwood wakiw awamevaa tena make up ambazo walitengenezwa na mtaalam mwingine walionekana kwenye Camera za CCTV za duka la Graff wakichungulia chungulia.lakini hakuna ambaye angeweza kuwatilia shaka sababu wakati huo huo gari la patrol la polisi lilipita kama mara mbili hivi katika mizunguko yake ya kiusalama.
HAWA WAHUSIKA WALIKUWA AKINA NANI.
Hii team ilikuwa imeundwa na jamaa wanne.Solomon Beyene mzaliwa wa Ethiopia huku kwetu Afrika.aliyekuwa na miaka 25 tu kijana mdogo ndo alikuwa ametoka Chuo na kabla ya hapo alikuwa amewekwa Segerea mwaka mmoja kabla ya tukio. Na huyu ndiye aliyekuwa amenunua simu kadhaa kwa ajili ya mawasiliano mbalimbali. Mpaka siku ya tukio alikwenda kukodi gari aina ya Ford ambalo lilitumika kuya block magari mengine katika harakati za kutoroka. Mahakama ilikuja kusema huyu inaonekana ndo alikuwa kiongozi wa tukio lile.
Alikuwepo Clinton Mogg aliyekuwa na miaka 43 mzaliwa wa Bournemouth huyu naye alikuwa mshiriki mzuri katika tukio hili.
Thomas Thomas huyu alikuw ana miaka 46 mzaliwa wa Kingston na Craig Calderwood aliyekuwa na miaka 27 ambaye yeye alikuja kudai kuwa alilazimishwa tu kushiriki lile tukio baada ya kuambiwa kama asingeshiriki basi yeye na mama yake wangeuawa na mtu ambaye anasema aliitwa “Kev” aliyejitambulisha kuwa yeye ni Big Boss.
WALIKAMATWA VIPI HAWA JAMAA.
Katika harakati za kutoroka wakiwa kwenye BMW waligongana na Cab moja amabyo iliwaziba njian na hapo wakapotez amud akidogo. Wakiwa katika hatrakati za kubadilisha gari kuingia lile gari la pili walisahau simu moja katikati ya seta ya dereva na ilipo handbrake. Walisahau pia bunduki aina ya shortgun yenye risasi na risasi nyingne kwenye boot ya gari. Wauzaji wa simu waliruhusu polisi waanze kutrack aliyenunua ile simu katik amaduka mbalimbali. Tarehe 20 Agost hawa jamaa walikuwa wameshapatikana na kufunguliwa mashtaka ya wizi, utekaji na kutishia maisha. Mpelelezi anasema kuwa wezi hawa walikuw awamejipanga vizuri kabisa wakijua ni wapi walikuwa wapeleke kwenda kuuza vile vito vya almasi. Pia walipanga tukio Hilo kwa ufundi wa hali ya juu sana. Kosa walilolifanya ni kusahau vile vitu hasa simu kwenye gari baada ya kuwa wamegongana na CAB na ule uharaka wa kutaka kubadilisha gari wakajikuta wamesahau vitu hivyo ambavyo polisi walitumia siku sizizodi 15 kuwakamata na kuwaleta katik avyombo vya sharia. Jamaa wali pewa nafasi ya kutumikia vifungo vyao katika segerea za huko kwao.
Mpaka dakika ya mwisho Kassaye alikataa kuwa yeye alikuwa ni mhusika mwenye asili ya afrika katika lile tukio. Akidai amesingiziwa tu na mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Omar. Craig Calderwood yeye alikubali kuwa alikuwa mhusika katik alile tukio ila alilazimishwa kama ambavyo alijitetea kule juu.
NINI LIKITOKEA KWA ZILE ALMASI?
Mpaka jamaa wanaenda mitamboni zile almasi hazikupatina na kwa mahesabu ambayo yalipigwa zilionekana kuwa na thamani ya Dollar Million 60 za Kimarekani. Mpaka septemba 2014 Almas zile zilikuwa zilikuwa hazijapatikana.Wataalam wanasema labda tayari zilikuwa zimeshakatwa katwa na kuuzwa kwa wateja au mteja aliyekuwa amekusudiwa au zilifichwa sehemu flani. Huo ndiyo wizi mkubwa kabisa wa Vito vya Thamani kwa kipindi hicho na wezi walifanikiwa ingawa walikuja kukamatwa kutokana na makosa kidogo ila vito vyenyewe havikupatikana na jamaa wanasubiria wamalize vifungo vyao watoke waje kugawana ikiwa hakuwagawana au tayari aliyekuwa big boss alishafanya yake nap engine kwa sasa ni mmoja ya matajiri wakubwa sehemu flani.
Baadhi ya picha za Vito vilivyoibwa Katika Duka la Almas La Graff

No comments:
Post a Comment